Jumatano 23 Julai 2025 - 00:21
Taifa la Iran halitaachana na heshima na akili

Hawza/ Hazrat Ayatollah Jawadi Amuli katika kikao na wanajumuiya wa kundi la Mu’talifeye Islami alisisitiza kwamba: Sisi ni warithi wa utamaduni na fikra ambazo si tu kwamba zilikuwa ni zenye kung’aa katika siku za nyuma, bali pia ni zenye kuongoza njia katika siku zijazo, taifa hili haliwezi kuachana na misimamo ya heshima, akili na utamaduni.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah al-Udhma Jawadi Amuli katika kikao chake na wanajumuiya wa kundi la Mu’talifeye Islami, huku akipongeza ripoti na huduma zilizotolewa, alieleza matumaini yake kuwa juhudi hizo zitakubaliwa mbele ya Mwenyezi Mungu, na mafanikio ya kutoa huduma bora zaidi kwa vizazi vijavyo yatapatikana.

Mtukufu huyo katika muendelezo wa mazungumzo yake aliashiria masiku ya maombolezo ya Bwana na kiongozi wa mashahidi, na akasisitiza juu ya ulazima wa kulielewa kwa ujuzi na kwa kina tukio la Karbala, akasema kwamba: "Tukio la Karbala kwetu ni kielelezo na mfano usio na kifani, na tunapaswa kuelewa vizuri sababu ya jambo hili," Ingawa suala la kulia na kuomboleza kwa ajili ya Sayyid al-Shuhada (as) lina nafasi yake, lakini kile kilichokifanya tukio la Karbala kuwa kielelezo na cha kudumu ni ujumbe wake wa kielimu na kimaarifa, ujumbe unaosema waziwazi kuwa lengo halihalalishi njia

مَنْ حَاوَلَ أَمْراً بِمَعْصِیةِ اللّه کَانَ أَفْوَتَ لِمَا یرْجُو وَأَسْرَعَ لِمَجِی‏ءِ مَا یحْذَر.

Yaani, iwapo mtu atataka kufikia malengo kwa njia ya kumuasi Mwenyezi Mungu, basi litampotea lile analolitarajia na litamjia kwa haraka lile analolikhofu. Ikiwa lengo ni la kimungu, basi njia ya kulifikia lazima iwe "ṣirāṭ al-mustaqīm" (njia iliyo nyooka).

Akinukuu juhudi za makhalifa wa Bani Umayyah katika kueneza fikra ya "jabriyyah" (kulazimishwa) na kuhusisha matukio na uhalifu wao wa kihistoria na irada ya Mwenyezi Mungu, alisema: "Bani Umayyah waliangaika kwa miaka mingi kueneza fikra ya kulazimishwa ili waweze kuhusisha jinai zao na Mungu, na kwa hivyo baada ya tukio la Karbala, Ibn Ziyad alimwambia Bibi Zaynab (as): “Je, umeonaje alilolifanya Mungu kwa ndugu yako?” – yaani, kitendo hicho alikihusisha na kazi ya Mwenyezi Mungu na si ya Shetani.
Bibi Zaynab alikabiliana na fikra hii ya "jabri" na mbele ya Ibn Ziyad akasema: “Sijaona isipokuwa uzuri tu.” Yaani, nyie ndio mliowaua, lakini kile ambacho Mungu alituamrisha kusimama dhidi ya dhulma tumekitekeleza, na mimi sioni chochote isipokuwa uzuri. Kauli hii ilikuwa ni tamko la kisiasa, kielimu na kiimani (tawḥīdi), si maneno ya kihisia tu.

Kiongozi huyu wa kidini alieleza kuwa: Harakati ya Hussein bin Ali (as) kwetu si tukio la fahari tu, bali ni msingi wa utambulisho wetu, hii si fahari ya kawaida, bali ni utambulisho wetu. Hata hivyo tunapaswa kuelewa kuwa taifa la Iran lenyewe pia ni taifa kubwa, Sisi watu wa Iran ni watu wakubwa, na wana wa wakubwa  Sisi, yaani watu wa Iran; ukizunguka Marekani nzima hutapata athari yoyote ya kale, lakini popote utakapokanyaga nchini Iran utapata athari za sanaa, historia, elimu na madhehebu ya fikra, hili ni taifa lenye mizizi na lenye utamaduni.

Mtukufu huyo akizungumzia mashambulizi ya kitamaduni kutoka Magharibi dhidi ya Iran, na akieleza kuwa mamlaka ya leo ya Iran ni matunda ya "basira" (utambuzi) wa taifa na ilhamu kutoka katika harakati ya Imam Hussein, alisema: Leo hii baadhi ya mataifa haya makafiri na wanaodai kuwa na maendeleo, kama vile Marekani na wenzake, wanayatusi mataifa ya Kiislamu na viongozi wetu wa kidini, lakini ukweli ni kwamba sisi ni warithi wa utamaduni na fikra ambazo si tu kwamba zilikuwa na uzuri uliong’aa katika siku za nyuma, bali pia ni zenye kuongoza njia katika siku zijazo, taifa hili si taifa ambalo kwa urahisi linaweza kuachana na misimamo ya heshima, akili na utamaduni.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha